Sunday, October 17, 2010

KARIBUNI CHUO CHA UHAZILI-MTWARA MJINI(MTWARA COMMERCIAL COLLEGE)

MKUU WA CHUO AKIPIPIGA 'LECTURE' DARASANI.....

UZURI WA HIKI CHUO UNAJIFUNZA SPIDI KWENYE 'TYPEWRITER'' KABLA HUJAANZA KUSHIKA COMPUTER, HIVYO HIKI CHUO NI MTAMBO WA KUZALISHA MASECRETARI WENYE SPIDI KWENYE KUANDIKA/KUCHAPA KWA COMPUTER.

(KWANI MASECRETARI WENGI MAOFISINI WANAONEKANA HAWANA SPIDI YA KUCHAPA YAANI NI MWENDO WA KOBE TU,NA IKITOKEA UMEME UMEKATIKA BASI NA KAZI IMELALA, HAWAWEZI KUTUMIA HIZI TYPEWRITER).


CHUO KIPO KATIKA HALI NZURI NA KINATOA MAFUNZO YAFUATAYO:

  • FULL SECRETARIAL DUTIES(SD)
  • OFFICE PRACTISE(OP)
  • ENGLISH STUDIES
  • COMPUTER STUDIES (ALL MICROSOFT OFFICE PROGRAMS, ADOBE PHOTOSHOP, INTERNET)

KIPO AFFILIATED NA VETA-KIPO LIGULA C, KWA JIONEE JUNCTION MITA 100 KUELEKEA BARABARA YA CHUNO.
KWA MAMOMBI TUMA:

MTWARA COMMERCIAL COLLEGE
BOX 655 MTWARA.
Email: mtwaracommercialcollege@yahoo.com
Simu: 0784578283
NYOTE MNAKARIBISHWA

KISA KILICHONITOA MACHOZI WAKATI NIPO MTWARA.

Kwa wale wakazi wa Mtwara,mtakuwa mnaijua vizuri ile barabara itokayo pale Ligula Hospitali inashuka chini kuelekea kwa Jionee, Cocobeach,TTC mpaka kiyangu, hii ni barabara kubwa na ina nzuri kwani ina kiwangi kizuri cha lami. Ukifika pale kwa jionee kuna junction, ile barabara inayoelekea CHUNO, na hapa ndipo kisa hiki kimelalia.

Hii barabara ilikuwa ipo kwenye service, labda inawezekana ukweli kwamba kipindi hiki cha uchaguzi mara nyingi barabara za huku mtwara nyingi zinafanyiwa marekebisho. Sasa Muhandisi wa hii barabara(Contractor) ni kijana flani wa makamu(miaka 35-40) simfamu kwa jina ila tu nikimwona mwona na wafanyakazi wengine wa barabara hii wakijishughulisha kuweka lami hii barabara.

Hivi majuzi huyu bwana, alitokea kumpenda(sidhani kama ni kumpenda au ni hulka ya mwili) mdada flani(jina nalihifadhi) ambae amepanga nyumba flani inatazama na hii barabara. ifahamike kwamba huyu dada alikaa zaidi ya miaka miwili hospitali na ni mwasirika wa VVU, na still anaendelea kutumia ARV kusogeza siku mbele, na hapo mtaani watu wote kama sio wengi wanamfamu vizuri tu huyu dada. Ikumbukwe kipindi cha nyuma miaka ya 2000 huyu dada kutokana na uzuri wake alikuwa 'matawi ya juu' sana!

Huyu Contractor bila kujua hilo(ni mkazi wa Dar) akaja siku hiyo pale kwake akamtongoza wakakubaliana, akalala nae.

Siku ya pili huyu bwana akaja tena, akanunua soda, akaket mduleni akaanza kunywa. Bahati nzuri mama mwenye nyumba siku hiyo alikuwepo pale na huu 'mchongo' alikuwa keshaupata. Basi yule mama nae akaenda kukaa na yule baba pale mduleni, na 'akamchana live' kwamba ulyefanya nae ngono jana ni muathirika ana UKIMWI......

Ngoja niwaambieni..huyu dada ni ''muuaji'' kiufupi,alicheza sana kipindi cha 'balehe' yake,labda kwa sababu ya uzuri wake. Wakati yupo hospitali manesi walikuwa wakisema aliruhusu kuingiliwa nje ya maumbile na kusababisha kupigwa 'bomba' na ikafikia hatua kwamba sehemu kubwa ya viungo vyake vya ndani(utumbo) vimeshaharibika, na isitoshe miguu yake imeshapoteza nguvu(haina balance), ni juzi tu alianguka kwenye ngazi za kupandia bafuni na kusababisha mguu wake mmoja kuvunjika na tayari keshawekwa kopa(POP).

Na yule daktari aliyemtibu huo mguu alikuja kumuangalia pale home kwake na baadae aliwaambia wapangaji wengine kwamba eti wakati anamweka kopa alikuwa anamtega kumshikashika' wakati yeye(dokta) ndiye aliyekuwaw anasupply ARV kwa huyoo dada. Isitoshe siku moja mtoto kiume wa mama mwenye nyumba aliitwa chumbani kwa huyu dada ili amkrekebishie TV yake,akampa na bia moja, jamaa akawa anakunywa, bia ilipofika nusu yule dada akaanza kumtega kumkumbatia n.k. Jamaa kuona hivyo akaruka na kuondoka zake. Baada ya masa kadhaa kupita jamaa akarudi amelewa na akaanza kumtusi yule dada ikawa kama kuna ugomvi hivi....so huyu dada anafanya makusudi kuwafata wanaume ilhali anajua yeye ni mgonjwa. Sina uhakika kama huyu Contractor alimtongoza au huyu dem alimtega na jamaa akaingia kichwakichwa...

Yule baba alivunja ile soda aliyekuwa anakunywa palepale, akaanza kulia na kutoa michozi huku akisema kwa uchungu kwamba alikuwa hakujua hilo, mbaya zaidi alisema kwamba kabla ya kukutana nae alienda duka la jirani kununua Condomz, lakini yule dada alikataa katakata kutumia kondom nna jamaa akaziweka kando....kikubwa zaidi wakati analia akisikika akisema kwamba ana mke na watoto, na hajui atamwambia nini mke wake akirudi huko Dar.

Baada ya siku mbili kupita tangu ule mkasa niliona magari ya mchanga yakija na kuanza kusomba zile changarawe ambazo ilibidi zitumike kwenye ile barabara na mpaka sasa hivi hii barabara ina changarawe zenye vumbi na ule uji wa lami haujawekwa bado, nilijaribu kuwauliza wale jamaa wakiopaikiza changanrawe kulikoni walisema yule contractor kaenda Dar es salaam..sasa sikujua kwamba mkataba kaukatisha au ilikuaw vp wameiacha hii barabara na vumbi lake...Hiki ni kisa cha kweli na kimeniskitisha sana .

JK KUMBE 'ANA-AKILI' MTWARA HATUHITAJI TENA MELI...

Ni kawaida kukuta hali hii ukiwa njiani.....sikupata taarifa kuhusu abiria wa gari hii...

Hapa ni Nangurukuru...Hata Maabasi ya NAJMA ni mapya kabisa kwa wale abiria wa Nachingwea!!,Mengine ni MAHUTA EXPRESS, THE BLUES_CHELSEA, BUTI n.k.Hey Mlio ughaibuni Mtwara Inapaa sasa hivi...Mabasi yanatoka stend ya Mtwara saa 2 asubuhi,na sio tena saa 11 alfajiri kama zamani...na yanafika Dar saa 9 alasiri.


SAFARI YANGU YA DAR ILIWEZESHWA NA HII 'BUS'
Mpaka Royal Coach zinatimba Mtwara..ila niwajuze tu,hili bus huduma zake za ndani sijazipenda!!Hawajaweza bado kushindana na bus za SUMRI na NG"ITU..humo ndani utapata soda,biscuits, keki...vilevile utasoma magazeti n.k. Hili bus ingawa ni 'ROYAL' lakini huwezi pata huduma hizi...!!

Wednesday, October 13, 2010

WAMUONA JK...SPANA(GLASS) MKONONI...!!


HUYU NDIE NTONDOLE MURJI...MANYABIASHARA WA KIHINDI MAARUFU SANA KANDA YA HUKU KUSINI...ALIWAHI KUWA MBUNGE MAENEO FLANI,LAKINI MPAKA LEO WATU WA HUKO HAWATAKI HATA KUMSIKIA.....TAFAKARI!!!

WAMUONA JK...SPANA(GLASS) MKONONI...!!

HUYU NDIE NTONDOLE MURJI...MANYABIASHARA WA KIHINDI MAARUFU SANA KANDA YA HUKU KUSINI...ALIWAHI KUWA MBUNGE MAENEO FLANI,LAKINI MPAKA LEO WATU WA HUKO HAWATAKI HATA KUMSIKIA.....TAFAKARI!!!
HUYU NDIE NTONDOLE MURJI...MANYABIASHARA WA KIHINDI MAARUFU SANA KANDA YA HUKU KUSINI...ALIWAHI KUWA MBUNGE MAENEO FLANI,LAKINI MPAKA LEO WATU WA HUKO HAWATAKI HATA KUMSIKIA.....TAFAKARI!!!

WAWEZA KUAMINI BAADA YA SHOW WATU WALITAWANYIKA KABLA JK HAJAFIKA?


BAADA YA SHOW ...WATU HAOOOOOOO..

JAMANI HUYU SIO MICHUZI ????

MARLAW,KOPA NA ALBINO NAO WAMO

Aagh mi' nilienda kuangalia 'VIDUKU" tu!!

HAYA NDIO MACOSTA YAKIYOSOMBA WATU TOKA PANDE ZA MJI..

DIAMOND ALI''WASHIKA'' WAKAZI WA MTWARA........!!
HATA KABLA YA MKUTANO HAUJAISHA...WATU HAO WANASUBIRI MILANGO IFUNGULIWE WAANZE KURUDI MAKWAO.........
BAADA YA KUSOMBA SANA WATU PANDE ZA ZIWANI, MIKINDANI, KIYANGA,CHUNO, MBAE,MKANGARA NA MAENEO MENGINE...HAYA MACOSTA YALIKUWA YANASUBIRI MKUTANO UISHE YAANZE KURUDISHA WATU. JIONEENI WENYEWE WAZEE.

Monday, September 13, 2010